Ilikuwa safari ya Siku mbili ambapo alifanikiwa kufika katika mji wa halale nchini Zimbabwe
Akiwa hafahamiani na MTU yoyote kijana Steve ikabidi atafute mahala ambapo anaweza kupata chakula maana alikuwa mida ya saa tisa alahasili
Kipindi anawaza wapi atapata chakula na ni chakula gani maana yupo nchi ya mbali alijitokeza kijana mmoja ambae akamuuliza Steve "are you from Tanzania?" Steve akamjibu "yes iam from Tanzania" baada ya kujibizana hivyo ndipo wakatambuana kuwa wote ni watanzania
Kilicho fuata ni maongezi ya hapa na pale Steve akamwambia yule kijana nipo safarini naelekea Afrika ya kusini nakwenda kutafuta maisha yule kijana akamjibu unamakubaliano na mtu yoyote kule? Steve akamjibu hapana
Kijana Huyo akamwambia Steve umefanya maamuzi magumu kwenda sehemu mbali na nyumbani ukiwa haumfahamu mtu yoyote Steve akamjibu kuwa hakuwa na jinsi ni lazma afanye hivyo
Baada ya Massa machache kijana huyo aitwae James akamsaidia Steve kupata tiketi ya kusafiri kuelekea Afrika ya kusini kwa njia ya basi kupitia mpaka wa beitbridge nimpaka unao tenganisha nchi ya Zimbabwe na south Afrika kupitia mto Limpopo Steve alianza safari Zimbabwe saa mbili usiku kuelekea Afrika kusini
Itaendelea.....
Mtunzi:Steve christian
0713861567