Urusi inalaumu shambulizi la Ukraine baada ya sehemu nzima ya ghorofa kuanguka kufuatia mlipuko huko Belgorod.
CCTV kutoka eneo la tukio inaonyesha mlipuko mkubwa karibu na msingi wa muundo wa ghorofa 10 na kisha jengo linaanguka.
Takriban watu 17 wamejeruhiwa na kuna ripoti za vifo na pia watu walionasa kwenye vifusi.
Mji huo wa Urusi uko karibu na mpaka na Kharkiv nchini Ukraine, ambapo wanajeshi wa Putin walianzisha mashambulizi siku ya Ijumaa.
Mkoa wa Belgorod mara nyingi umekuwa ukilengwa na vikosi vya Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mnamo 2022, lakini hakujakuwa na neno kutoka upande wa Ukraine juu ya tukio la hivi punde.
Hapo awali, maafisa wa Kyiv walisema mashambulizi ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na la Belgorod, hayalengi raia.