Baada ya kutoka garage kwa mjomba wake Steven akaanza mipango ya kutimiza ndoto yake ya kufika barani ulaya hususani nchini uingereza au America
Alijikusanya na kufanikiwa kupata pesa ya nauli na pesa ya matumizi machache ili kukamilisha safari yake ya kufika barani ulaya
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kwenda kuomba VISA kwenye ubarozi wa uingereza anbako alitakiwa kufanyiwa mahojiano na bahati mbaya hakufanikiwa kupata vigezo vya kupatiwa VISA
Baada ya kufeli alikaa chini na kuwaza ndipo akapata wazo jipya kuwa aende nchini Afrika ya kusini baada ya kushindwa kupata vibali vya kuingia uingereza
Aliamua kwenda Afrika ya kusini kwakuwa RAIA wa Tanzania wanaingia bila vikwazo nchini humo ilimladi wawe na pasi ya kusafiria tuu
Akiwa hafahamiani na mtu yoyote nchini Afrika ya kusini kijana Steve aliamua kuchukua uamuzi wa kwenda huko.
Alianza safari ya kwenda nchini Afrika ya kusini kwa usafiri wa basi LA kampuni ya "Takwa" ambalo linafanya safari za Tanzania mpaka Halale nchini Zimbabwe kupitia mpaka wa tunduma ......
INAENDELEA...
Mtunzi:Steve christian
0713861567