JOSHUA NASSARI APELEKA USHAHIDI MWINGINE TAKUKURU

Mbunge wa jimbo arumelu  Joshua nasari jana aliwasilisha ushahidi wake mwingine TAKUKURU kuhusu tuhuma.za kutoa rushwa zinazo fanywa.na CCM

mbunge huyo aliwasili ofisini hapo majira ya saa saba mchana na kuondoka majira ya saa kumi na moja

baada ya kutoka maafisa wa TAKUKURU waliwafukuza wana habari na hawa kuruhusu mbunge huyo aongee nao maeneo hayo

kipindi anatoka alisindikizwa na.mmoja wa maafisa wa takukuru mpaka kwenye gari lake na kuhakikisha ameondoka kabisa

lakini yeye aliwataka wana habari kuja sehemu nyingine ili aongee nao kuhusu ujio wake

akiongea na wana habari alisema amekaa kwa muda mrefu ni kutokana na ushahidi wake kuwa mpana

alisema amewasilisha ushahidi wa kutosha na amesha fungua jarada la kesi hiyo na majukumu mengine kawaachia wao TAKUKURU wafuate taratibu zao

Post a Comment

Previous Post Next Post