Katika mapenzi kila mtu ana kigezo cha kumpata mpenzi anayempenda. Msanii wa Bongo Fleva, Shilole ametaja sifa za Mwanaume anaempenda na kusema kuwa anavutiwa sana na Wanaume warefu kuliko wafupi.
Shilole amesema anampenda Mwanaume yoyote yule anaejitambua ingawaje kidogo sifa za nje awe mrefu kwani hana hisia zozote kwa mwanaume mfupi.
“Mimi napenda mwanaume yoyote yule ilimradi anajitambua basi, suala la muonekano hilo linatengenezwa ila kiukweli kabisa mimi napenda mwanaume mrefu, mwanaume mfupi kwangu hapana,Sipendi Wanaume wafupi, Barnaba yeye ni mfupi na kila mmoja ameumbwa na Mungu tofauti, ila sasa hivi vigezo na masharti kuzingatiwa“Alisema Shilole kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV.
Hata hivyo Shilole ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa anatamani sana kuolewa kwani ndoa ni heshima kwa mwanamke .
“Hamna mtu asiyependa kuolewa, ndoa ni heshima ndiyo maana unasikia watu wanasema mke wa fulani yule, muwe wa fulani yule lakini siyo aah yule si mwanamke tu kwa hiyo ndoa ni heshima” alisema Shilole.