Kagera sugar yaapa kumfanyia Azam fc kama alichofanyiwa simba

maishanasheria
By -
0
Kocha msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangalu amejitapa kuwa kikosi chake kipo imara kupambana na Azam FC mwishoni mwa juma hili huku akidai watapambana kuhakikisha wanabakia katika nafasi ya tatu ndani ya msimamo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo amesema ijapokuwa ligi imekuwa ngumu lakini wana matumaini makubwa ya kuwafunga wapinzani wao Azam FC waliowatangulia nafasi moja mbele katika msimamo wa ligi.
“Wachezaji wangu wote kiafya wapo vizuri, tangu tumeanza Ligi tumekuwa washindani mpaka hii leo tupo nafasi ya nne tukiwa tumepishana pointi mbili na wapinzani wetu Azam FC ambao wapo nafasi ya tatu na tunataka tushindane ili tuipate nafasi ya tatu. Kwahiyo tutafanya kile kile tulichokifanya kwa Simba. Alisema Jangalu kwenye mahojiano yake na swahibanewz 
Mchezo huo wa kukata na Shoka utachezwa Jumamosi kunako dimba la Azam Complex.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)