Rasmi Ndoa ya Yanga na Chama Yafika Mwisho, Hawamuongezei Mkataba
Taarifa za uhakika kutoka katika chanzo cha kuaminika cha habari za michezo nchini Tanzania zinaeleza kwamba klabu ya Yanga Sc imefikia makubaliano ya kuachana ramsi na aliyekuwa kiungo mshambuliaji wao raia wa nchini Zambia Clatous Chota Chama.
Chanzo cha taarifa hii kimeeleza wazi kwamba mkataba wa Chama ndani ya klabu ya Yanga Sc umemalizika rasmi na viongozi wa klabu hiyo hawana mpango wa kumuongeza mkataba mpya kutokana na sababu za kimaslahi.
Inaelezwa kwamba Chama alihitahi kupewa ofa nono ya mkataba mpya ili aendelee kusalia katika klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa msimu mmoja pekee lakini viongozi wa klabu ya Yanga Sc hawakuwa tayari kukubaliana na mahitaji ya Chama badala yake wamemruhusu akatafute changamoto mpya kwenye klabu nyingine.
Chama anaamini kwamba bado anaweza kuwa mchezaji muhimu ndani ya klabu ya Yanga Sc na ndio maana aliweka mezani ofa kubwa ili aweze kupewa kandarasi mpya ya kuendelea kuwatumikia wananchi kuelekea katika msimu ujao wa mashindano