Tottenham, Newcastle na Napoli zote zinamfuatilia kiungo wa England Jack Grealish baada ya Manchester City kuweka bei ya pauni milioni 40 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 (Sun).
Newcastle United wanaendelea kuwa na matumaini ya kushinda mbio za kumsajili Marc Guehi, 24, huku klabu hiyo ikitaka kuimarisha kikosi chao kwa kumuongeza beki wa kati huyo wa England na Crystal Palace (GiveMeSport).
Crystal Palace wenyewe wako kwenye mazungumzo na Sporting kuhusu uwezekano wa mpango wao wa pauni milioni 45 kumnasa beki wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 21 (Guardian).
Newcastle pia wamefanya mazungumzo mapya na Dominic Calvert-Lewin, 28, huku meneja Eddie Howe akiwa shabiki wa muda mrefu wa mshambuliaji huyo wa England aliyeondoka Everton baada ya mkataba wake kumalizika mwezi uliopita. Anasakwa pia na maslahi kutoka Manchester United (Talksport).