Kwa muda mrefu watu wengi waliaminishwa kuwa katikati ya nchi ya tanzania ni dodoma kumbe siyo dodoma
akijibu swali bungeni naibu waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi mh Angelina mabula akijiby swali aliloulizwa ni lini nchi italisibitisha enei la chisinjisa kuwa ni katikati ya nchi?
waziri alisema kiukweli mpaka sasa serikali haijui katikati ya tanzania ni wapi ingawa kuna mwaka wanasiasa walisema kuwa ni kijiji cha mhalala mkoani singida
alisema serikali haina jibu kamili ni wapi katikati ya tanzania mpaka sasa na wapo mbioni kuanza uchunguzi ili waweze kuja na majibu sahihi
kwa miaka mingi watu waliamini dodoma ndiyo katikati mwa tanzania hatua ambayo mh naibu waziri ameikanusha
pia kuhusu lini wataanza kupima waziri amesema mpango huo upo chini ya wizara na wanatarajia pia kufanya hivyo ila ni kwa siku zijazo na siyo hivi karibuni
Tags
Kitaifa