wakimbizi watoto wa sudani kusini waingia uganda

Jumla ya watoto wakimbizi ambao
wamepotezana na wazazi wao ni 729 ambao
wamekimbilia Uganda kufuatia
mashambulizi mapya Sudan Kusini.
Kati ya wakimbizi hao (watoto), 570
walitenganishwa na wazazi wao kutokana na
kuanza kwa vita na kukimbilia maeneo tofauti
na wengine 159 wamepoteza mawasiliano na
ndugu zao ambao walikuwa wakikaa nao
kabla ya vita kuanza.
Watoto ambao wako kwenye upweke ni
wenye umri kati ya miaka minne na kumi na
saba.
Kwa mujibu wa kamanda wa makazi ya
wakimbizi ya Palabek David Wangwe, watoto
hao wamekabidhiwa kwa wazazi wa kufikia
ambao wanawangalia kwa hivi sasa.
“Resheni za chakula na mahitaji mengine
yaliyokusudiwa kwa watoto hao yanatolewa
kwa wale walipewa jukumu la kuwatunza
watoto hao.
Vyanzo vya habari nchini Uganda vimesema
kuwa mipango iko njiani amesema Wangwe
kutoa vifaa vya kujifunzia kwa watoto hao ili
shule zitakapo funguliwa waweze kuanza
masomo.
Repoti ya Umoja wa Mataifa
Wakati huo huo Repoti ya Umoja wa Mataifa
(UN) imesema kuwa majeshi ya upande wa
serikali ya Sudan Kusini yameua watu 114 kati
ya Julai 2016 na Januari 2017 katika mji wa Yei.
Repoti hiyo ya Kitengo cha Haki za Binadamu
cha Shughuli za UN nchini Sudan Kusini
(UMNISS) na ofisi ya Haki za Binadamu ya UN
imetolewa Ijumaa.
Repoti hiyo pia “inafichua matukio ya
wananchi kupigwa mabomu bila ya
kutenganisha kuwa sio askari; mauaji yenye
kuwalenga; kuibiwa mali zao na kuchomwa
kwa mali za raia pamoja na vitendo vya
ubakaji vinavyoendeshwa dhidi ya wanawake
na wasichana, wakiwemo wale ambao
wanakimbia vita.”
UN imesema kuwa makosa haya ya jinai “
yanaweza kufikia kuwa jinai ya kivita dhidi ya
binadamu” na kuidhinisha uchunguzi wa kina.
Repoti hiyo imesema kuwa mapigano
yamezuka wakati majeshi ya upande wa
serikali yalipokuwa yakimsaka mpinzani wa
Rais Salva Kiir ambaye aliwahi kuwa naibu
wake Riek Machar. “Mapigano hayo yalitokea
eneo ambalo alitorokea,” waraka huo
umeeleza.
Yei ilikuwa ni “mji wenye amani kwa sehemu
kubwa,” UN imesema, ikiwa na wakazi kati ya
200,000 na 300,000 wa makabila tofauti.
Mapigano haya yamesababisha mpasuko
mkubwa kati ya makabila na kupelekea watu
kulengwa kuuawa, kukamatwa, kubakwa na
makundi ya raia kusukumwa nje ya makazi
ikakidiriwa kuwa nusu ya watu wanaoishi
katika mji huo.
Repoti hiyo inasema kuwa mgogoro wa Yei “
kwa mara nyengine unaonyesha kuwepo kwa
mwanya uliosababisha wimbi la uvunjifu wa
amani linaloendelea kote nchini Sudan Kusini.
Sudan Kusini imekumbwa na vita vilivyoingia
mwaka wan nne tangu mapigano yaanze kati
ya zinazo msaidia Kiir na wale wanaompinga
Desemba 2013.
UN imesema zaidi ya wananchi milioni 1.8 wa
Sudan Kusini wamekimbia nje ya nchi na
wengine milioni 1.9 wamepoteza makazi yao
kutokana na vita.


Post a Comment

Previous Post Next Post