irani yaanza kuhesabu kura

Zoezi la kuhesabu kura
limeanza nchini Iran leo
Jumamosi baada ya wapiga
kura kujitokeza kwa wingi
katika uchaguzi ambao bila
kutarajiwa umekuwa wenye
mvutano mkubwa baina ya
rais wa sasa Hassan Rouhani
, ambaye anataka kurejesha
mahusiano ya kawaida na
mataifa ya magharibi, dhidi
ya jaji mwenye msimamo
mkali ambaye anasema
kwamba rais wa sasa tayari
amekwenda mbali mno.
Wapiga kura wakipiga kura zao
nchini Iran katika uchaguzi wa
Ijumaa Mei 19, 2017
Zaidi ya wapiga kura milioni
40 walipiga kura, imesema
wizara ya mambo ya ndani ,
ikiashiria kwamba watu
waliojitokeza wanafikia
asilimia 70 katika uchaguzi
uliofanyika jana Ijumaa ,
karibu sawa na jinsi watu
walivyojitokeza kupiga kura
katika uchaguzi wa mwaka
2013 wakati Rouhani
alipoingia madarakani kwa
ushindi wa kishindo.
Upigaji kura ulirefushwa
kwa masaa sita kwasababu
watu wengi bado walikuwa
katika mistari. Magazeti
nchini Iran yamesifu jinsi
watu walivyojitokeza kupiga
kura, yakiandika vichwa vya
habari kama "ushindi wa
kihistoria kwa Wairani".
Kasi ya mabadiliko
imekuwa ndogo
Wapiga kura nchini Iran
Tovuti za habari zinazounga
mkono mageuzi zimesema
Rouhani alikuwa mshindi.
Hata hivyo hawakutoa
ushahidi, lakini watu
kujitokeza kwa wingi
kunaweza kuelemea upande
wa Rouhani, ambapo wasi
wasi mkubwa wa waungaji
wake mkono ni kuchoshwa
miongoni mwa wapiga kura
wanaopendelea mageuzi
waliovunjwa moyo na kasi
ndogo ya mabadiliko.
Rouhani , mwenye umri wa
miaka 68, ambaye aliingia
madarakani akiahidi kuiweka
Iran karibu na mataifa
ulimwenguni na kuwapa raia
wake uhuru zaidi nyumbani ,
anakabiliana na upinzani
mkali bila kutarajia kutoka
kwa Ebrahim Raisi mwenye
msimamo mkali, anayeungwa
mkono na kiongozi mkuu
nchini humo Ali Khamenei.
Uchaguzi huo ni muhimu
"kwa hali ya baadaye ya
jukumu la Iran katika eneo
hilo na dunia kwa jumla",
Rouhani , ambaye alipata
makubaliano na mataifa
makubwa yenye nguvu
kuiondolea nchi hiyo
vikwazo vya kiuchumi,
alisema baada ya kupiga
kura.
Wakati wa kampeni ya urais
nchini Iran
Raisi mwenye umri wa miaka
56 , amemshutumu Rouhani
kwa kuuvuruga uchumi wa
nchi hiyo na amesafiri hadi
katika maeneo wanakoishi
masikini, akizungumza katika
mikutano akiahidi mafao
zaidi ya kijamii na ajira.
Matokeo
yataheshimiwa
Anaaminika kuwa anaungwa
mkono na majeshi yenye
ushawishi mkubwa nchini
humo ya walinzi wa
mapinduzi, pamoja na
uungwaji mkono mkubwa
wa kiongozi mkuu nchini
humo Khamenei, ambaye
madaraka yake yanapindukia
yale ya rais aliyechaguliwa
ambae lakini kwa kawaida
hujiweka mbali na shughuli
za kila siku za kisiasa.
"Naheshimu matokeo ya
kura za wananchi na
matokeo yataheshimiwa nami
pamoja na wananchi," Raisi
alisema baada ya kupiga
kura, kwa mujibu wa shirika
lisilokuwa rasmi la habari
Fars.


Post a Comment

Previous Post Next Post