MWANAMKE AFANIKISHA KUPANDA MLIMA EVEREST

Anshu Jamsenpa, 37, ambaye ni mama wa watoto
wawili, alifika kileleni tarehe 16 Mei na akarejea
tena 21 Mei, afisa wa utalii Gyanendra Shrestha
ameambia Idhaa ya BBC ya Kinepali.
Rekodi ya sasa ya dunia ya Guinness ya kuupanda
mlima huo mara mbili kwa kasi zaidi ni ya siku saba
kwa wanawake.
Habari za mafanikio hayo ya Jamsenpa
zimetangazwa huku kukiwa na habari za tanzia,
baada ya wapanda mlima zaidi ya watatu kufariki
wakiukwea mlima huo mwishoni mwa wiki.
Mpanda milima kutoka Australia alifariki akikwea
mlima huo kutoka upande wa Tibet naye raia wa
Slovakia na Mmarekani wakafariki upande wa
Nepal.


Post a Comment

Previous Post Next Post