Mgahawa mmoja mjini London umekumbwa na
habari bandia za kuuza nyama ya mtu.
Wafanyikazi katika mgahawa wa Karri Twist katika
eneo la New Cross nchini Uingereza
wamehangaishwa kwa kupigiwa simu kutoka kwa
wateja wanaosema ''Kwa nini hamujafunga''?.
Mgahawa huo wa chakula cha jioni ni mwathiriwa
wa habari za mzaha zilizodai kwamba mmiliki wake
alikamatwa kwa kuweka nyama ya binadamu katika
chakula na kwamba miili 9 ilipatikana katika jokovu
la mgahawa huo.
Na watu wengine waliamini mzaha huo.
Habari hiyo ilichapishwa katika chombo cha habari
cha channel23news.com, mtandao ambao wateja
wake wanaweza kuchapisha habari za uwongo ili
kuwafanyia mzaha rafiki zao kwa kuchapisha moja
kwa moja katika mtandao wa fecbook.
Tags
Entertaiment