dereve wa mwendokasi kizimbani baada ya kumkata kidore abilia






Dereva wa basi la Mwendokasi, Khalid Shaha (43), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam, akikabiliwa na shtaka la kumkata kidole Godfrey Liwa kwa kioo cha gari.



Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Hanifa Mwingira, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Matarasa Hamisi, alidai Oktoba 12 mwaka jana eneo la Magomeni, Wilaya ya Kinondoni, dereva huyo alimkata Liwa kwa kioo cha gari.



Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na aliachiwa kwa  dhamana hadi Machi 12, mwaka huu kesi itakapotajwa tena.


Post a Comment

Previous Post Next Post