Bilionea wa Urusi aliyezaliwa nchini Uzbekistan
Alisher Usmanov amewasilisha ombi la pauni bilion
moja kuinunua Arsenal kutoka kwa mmiliki wake
Stan Kroenke.
Huku Kroenke akiwa hana hamu, ombi hilo
limekataliwa ijapokuwa Usmanov hajapata
uthibitisho woote kupitia maandishi.
Gazeti la The Financial Times limeripoti kamba
Usmanov aliwasilisha ombi hilo mwezi uliopita na
kwamba Kroenke hajatoa tamko ramsi kuhusu ombi
hilo.
Mfanyibiashara huyo wa vyuma anamiliki asilimia
30 ya hisa za Arsenal.
Hatahivyo hayuko katika bodi ya kufanya maamuzi
ya klabu hiyo.
Usmanov alisema mnamo mwezi Aprili kwamba
Kroenke anafaa kulaumiwa zaidi kwa kushindwa
kufanya vizuri kwa klabu hiyo.
Arsenal inatengemea vilabu vyengine ili kuweza
kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa
mara ya kwanza baada ya miaka 21.
Arsene Wenger ambaye amekuwa kocha wa klabu
hiyo tangu 1996 amekuwa akizomwa na baadhi ya
mashabiki wa klabu hiyo kutokana na msusruru wa
matokeo mabaya.
Tags
Michezo