Kuna baadhi ya Simu huwa zina speed ya 2G ambayo ni kasi ya chini sana, na ungependa kuweka 3G, umejaribu njia nyingi hata kwa kuhamisha SIM Card lakini umeshindwa, Sasa unaweza uka command ili kuweka 3G au 4G kwa kufuata njia nilizokuwekea hapo chini. Kabla ya yote je, Unajua Internet?
Internet ni kitu cha muhimu sana na ambacho karibu watumiaji wote wa smartphones hukizingatia kwanza. Lakini kuna baadhi ya watumiaji wa smartphones wamekuwa wakikubwa na matatizo ya simu zao kutomuwa na mtandao wa internet ambao haueleweki mara 2g mara 3g, 4g pasipo ruhusa ya mtumiaji.
UNAJUA KWA NINI HALI HII HUTOKEA?
Frequencies za mtandao hubadilishana kutokana na matumizi ya internet kwenye eneo husika, hivyo suala la smartphone kujichagulia mtandao yenyewe hutegemeana frequencies za mtandao upi unaokuwa na nguvu ndani ya muda husika.
Kama frequencies za 2g, 3g au 4g Zitakuwa na nguvu basi smartphone yako itakachagua mtandao wa kutumia yenyewe.
KAMA SMARTPHONE YAKO INAJICHAGULIA 2G, 3G, AU 4G BILA WEWE KUPENDA BASI FANYA YAFUATAYO
Kwa Simu za Android
NENDA SEHEMU YA KUANDIKIA NAMBA
BONYEZA >>> *#*#4636#*#* kama inakataa download application ya Phone testing
Yatatokea machaguo kadhaa chagua #Phone information
Shuka chini kabisa mpaka mpaka sehemu iliyoandikwa Set preferred network type gusa chini yake utaona machaguo ya mtandao yenye kumanisha aina ya mtandao wa internet.
Chagua:
GSM only kwa 2G peke yake
WCDMA only kwa 3G peke yake
LTE only kwa 4G peke yake
ZINGATIA HAYA:
Njia hii inafanya kazi kwenye simu nyingi za android lakini baadhi ya smartphones kama Samsung inakataa. Hivyo kama una simu ya jinsi hii na unatumia Android fanya rahisi ifuatavyo:
Nenda kwenye Settings za simu
Angalia kipengele cha Network
Chagua Mobile network
Bofya Network mode
Yatatokea machaguo ya mitandao ya internet kulingana na uwezo wa simu yako yaani 2G, 3G, na 4G.
KWA SMARTPHONE ZINAZOTUMIA WINDOW
Nenda sehemu ya kupigia simu
Bonyeza ##3282 au ##3282#
Bofya kwenye kwenye […] vidoti 3
Kisha chagua mtandao unaotaka kufanya simu yako iutumie muda wote yaani >> 2G, 3G, au 4G.
JINSI ya kuweka 4G kwenye simu yako
By -
June 17, 20212 minute read
0
Tags: