Jinsi ya kurudisha picha au video zilizofutwa kwenye simu ya Android

Admin
By -
0




Fikiria una kesi inaunguruma mahakamani na ushahidi pekee wa kesi hiyo unao kwenye simu (message au picha), bahati mbaya unaifuta hiyo message au picha bila kukusudia na hujui namna ya kuirudisha hapo nadhani utakuwa katika hudhuni kubwa sana.
Au una ujumbe unaothibitisha muala (transaction) fulani wa fedha na unaufuta kwa bahati mbaya.
Hii inatukuta sana hasa tunapokuwa katika mazingira fulani ya uwoga au presha na kujikuta tukipoteza baadhi ya vitu vya muhimu kama picha za familia zetu, message zetu au video.
Ondoa shaka, RAFAS NEWS tunakupa maujanja ya jinsi ya kurudisha picha, message, video au mafaili yako ya muhimu yaliyopotea au uliyoyafuta bila kukusudia kwa msaada wa Android SmS Recovery Tool.
NOTE:
  • Kifaa chako lazima kiwe kimerootiwa (Root Access) ili kuweza kutumia application hii. Kuroot ni kujipa uwezo wa kucontrol kifaa chako kwa 100% na kuna software nyingi zinazosaidia katika kufanya hili.
  • Pale unapofuta message au picha yako jitahidi usipokee au kutuma kitu kingine ili sehemu ya ile message iliyofutwa isijekuchukuliwa na kitu au message mpya itakayoingia (over written) na italeta ugumu katika kurecover (kurudisha) hiyo message au picha au inawezekana isiweze kujirecover tena.
Hebu tuangalie kwa kifupi nini huwa kinatokea pale tunapofuta picha, video, ujumbe (message) au faili lolote katika vifaa vyetu vya kuhifadhia kama diski hifadhi au SD Cards.
Faili lolote katika vifaa vyetu kama simu na kompyuta hutunzwa katika Diski Hifadhi ambazo zipo kwenye simu zetu, inaweza ikawa ROM au SD Card (Memory Card), kinachotuwezesha kuona mafaili haya katika programu endeshi kama photo viewer au Gallery ni link (uzi) unaounganisha (locate) sehemu lilipohifadhiwa faili hilo katika diski husika. Pale unapofuta faili lako kinachofutwa ni ule uzi (ile linki) na lile faili linabaki palepale, sasa tunaporecover kikubwa kinachofanyika ni kurudisha ile link (uzi) ili kuweza kuliona tena faili letu.

Njia za kufuata katika kuhakikisha unarudisha mafaili yako yaliyofutwa
Step 1
Step 2
  • Baada ya kudownload install hiyo Android recovery tool kisha irun (run it).
  • Chomeka simu yako kwenye Laptop au kompyuta yako kwa kutumia USB Cable.
  • Ruhusu USB Debugging kwenye simu yako kwa kwenda kwenye Settings–>Developer options–>USB Debugging.
recover-1
Step 3
  • Simu yako itaonekana katika Recovery Tool pale tu utakaporuhusu USB Debugging, bonyeza start button na software itaanza kuikagua (analyse) simu yako kisha bonyezaallow katika simu yako ili kuruhusu za zoezi kuendelea. Kumbuka unaweza chagua aina ya mafile unayotaka kuscan.
  • Kutunza muda, nenda moja kwa moja kwenye aina ya faili unalotaka na alafu chagua “scan for deleted files”.
recover-sms-02
Step 4
Subiri mpaka zoezi likamilike, muda wa kukamilika hutegemea sana na aina ya file unalotaka kulirudisha. Baada ya hapo software itakuletea ujumbe wa kukamilika kwa zoezi na itakuonyesha mafaili yote iliyorecover.
Message zote zilizofutwa zitaonekana katika ranginyekundu wakati zile zilizopo katika simu zitaonekana na rangi nyeusi, right click hizo message nyekundu kisha bonyeza “Recover”.
recover-message-from-android
Hapo utakuwa umemaliza, hakuna stress tena. 
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)