Baada ya masaa kadhaa kijana Steven alifika katika mpaka wa nchi ya Zimbabwe na Afrika ya kusini ambapo alifuata taratibu zote za kuvuka mpaka kwakuwa alikuwa na nyaraka zote zinazo mruhusu kuingia Afrika ya kusini
Ndipo safari ikaendelea na hatimae saa kumi na mbili hasubui akawa amewasili Johannesburg park station
Kama ilivyo kawaida abilia wote wakashuka kwenye basi na ndugu zao waliokuja kuwapokea wakawa wamewapokea lakini ilikuwa tofauti kwa Steven maana hakuna aliye kuwa anahamiana nae kwenye nchini ya Afrika kusini
Ikabidi atoke nje ya kitua cha basi huku akiwa hajui wapi pakwenda kwakuwa alikuwa ni mgeni na alikuwa na pesa chache kiasi cha Randi miatatu tuu wastani wa kama tsh 70000.
Baada ya kusimama saana huku akiwa hajui wapi pa kwenda ndipo akatokea RAIA mmoja wa Kenya ambae kwa haraka tu alivyomwona Steve akamjua kuwa ni mtanzania
Mkenya Huyo akamsogelea Steven huku Steven akiogopa akizani anataka kupolwa kwakuwa alishawai kuambiwa kuwa Afrika ya kusini kuna matukio mengi ya kupolwa
Mkenya alizidi kumsogelea Steven ndipo Steven akawa anaingiwa na hofu huku akirudi nyuma mkenya akamwambia usiniogope Mimi ni RAIA mwema tuu na ajamuuluza wewe ni mtanzania..? Steve akamjibu ndiyo Mimi ni mtanzania
Ndipo nae akajitambulisha kuwa ni mkenya na unaishi hapa kwa miaka mitano sasa akamuuliza Steve he una ndugu hapa..? Steve akamjibu hapana sina ndugu nimekuja kutafuta maisha na nahitaji msaada
Mkenya yule akamjibu usiwaze Mimi nitakupeleka mtaa unaitwa Ibrow huko kuna watanzania wengi lazma watakusaidia tuu
Baada ya maongezi machache ikaanza safari ya kuelekea ambako alimuhaidi atapata msaada kutoka kwa watanzania wenzake….
INAENDELEA…
Mtunzi:Steve christian
0713861567