MAHAKAMA YAWATIA HATIANI WAZUNGU WAWILI KWA KUKUSUDIA KUUA

Admin
By -
0

Middelburg, Afrika Kusini. Mahakama mjini hapa inatarajia kuwahukumu kifungo wazungu wawili baada ya kuwapata na hatia ya kujaribu kuua kwa kukusudia kwa kumtia ndani ya jeneza Mwafrika kisha wakatishia kuchoma moto.

Mchakato wa kuwahukumu umefanyika leo Jumatatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Middelburg baada ya kupatikana na makosa sita kati ya saba waliyoshtakiwa nayo Agosti 2017.

Chumba cha mahakama kilijaa huku wanaharakati na wawakilishi kutoka baadhi ya vyama vya siasa walifika kushuhudia hitimisho la kesi hiyo iliyoishtua nchi.

Tukio hilo lilizua gumzo kubwa nchini baada ya picha zilizopigwa kwa kutumia simu ya mkononi kusambazwa kwenye mitandao zikionyesha wakulima hao wa kizungu wakimsukuma Victor Mlothshwa, mkazi wa eneo hilo asiye na ajira akisukumizwa kuingia ndani ya jeneza Agosti 2016.

Picha hizo ziliwaonyesha wazungu hao, Willem Oosthuizen na Theo Martins Jackson wakijaribu kufunika mfuniko wa jeneza kwa mabuti yao huku Mlothshwa akililia uhai wake.

Pia watu hao walisikika wakimrushia matusi na wakitishia kummwagia mafuta ya petrol na kumchoma moto.

Tukio hilo lilifanyika katika shamba karibu na kituo cha umeme cha Komati kaskazini mashariki mwa Middleburg na kusababisha hasira, hali iliyoibua enzi za ubaguzi wa rangi.



Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)