Utapeli kutumia simu za mkononi kuendelea kudhibitiwa

Admin
By -
0
MATAPELI wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu kwa makosa ya kudukua taarifa za wateja wa huduma ya kifedha ya Tigo Pesa inayotolewa na kampuni hiyo  ambapo wamekuwa wakiwatapeli wateja wa kampuni hiyo ya Tigo kwa kujitambulisha kama wafanyakazi halali wa Tigo wakati si waajiriwa wa Tigo.
Matapeli hao hutumia mbinu hiyo kujipatia taarifa za siri za wateja hao ambazo baadaye wametumia kuiba kiasi cha fedha zipatazo shilingi milioni 26 kutoka kwa wateja mbalimbali wa mtandao huo kupitia huduma ya Tigo Pesa.
 
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, watu hwa wana mbinu mbalimbali kamakumpigia mtu simu wakisema aidha wamekutumia hela kimakosa kumpigia mtu simu wakidai ni makao makuu ya kampuni ya simu husika na wangependa utatue tatizo ambalo mteja fulaniamelalamikia.
 
Wakala mmoja aliyetajwa kwa jina la Amos Chirwa kutoka Kijichi, jijini Dar es Salaam, alisema matapeli ni wengi, na kila siku wanabuni njia tofauti ili waweze kuwaibia mawakala au wateja.
 
“Mimi kama wakala, ambae nina uzoefu wa miaka sita sasa, ningependa kuwashauri Watanzania kwa ujumla, kwamba usimpe mtu namba yako ya siri, au taarifa binafsi hata kama amejitambulisha kama mfanyakazi wa kampuni za simu kama Vodacom, Airtel, Tigo au Zantel, ” anasema wakala huyo akimalizia kwamba mtandao huo ungependa pia kuwaasa Watanzania kutojishirikisha na masuala ya kihalifu hususan katika masuala ya simu za mkononi kwani serikali ina mkono mrefu.
Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)