Bosi Mofaya ya Kiba kutua Bongo!

Admin
By -
0



UKITAJIWA kinywaji cha Mofaya, moja kwa moja jina la staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ litakujia na kusema kinywaji hicho ni chake.  Kinywaji hicho kinachoongeza nguvu (energy drink) kimejizolea umaarufu mkubwa nchini kupitia Kiba ambapo mwaka jana Klabu ya Mpira wa Miguu ya Coastal Union ya Tanga ilipata udhamini wa Mofaya. Usichokijua nyuma ya pazia ni kwamba, mmiliki wa kinywaji hicho ni Sbusiso Leope wengi wanamfahamu kama DJ Sbu akiwa ni DJ maarufu kutoka Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
UJIO WAKE
Ukiweka pembeni kinywaji cha Mofaya, DJ Sbu amefanya mengi nchini Afrika Kusini kupitia vitu mbalimbali kama ujasiriamali, uandishi wa vitabu na uhamasishaji huku akiwa tegemeo kubwa la vijana katika kutoa misaada mbalimbali.
Kwa mara ya kwanza DJ huyu anatarajia kutua Bongo leo (Jumatatu) na kesho (Jumanne) kuzindua kipindi maarufu cha radio cha Afternoon Drive kitakachoruka moja kwa moja kutokea mjengoni Global Group, Sinza-Mori jijini Dar.
Ikumbukwe kuwa, Sbu kwa upande wa burudani anashirikiana na Kampuni ya Times Media Group ya nchini Afrika Kusini na amefungua bonge moja la radio ya mtandao ya Massiv Metro ambayo inawafikia zaidi ya wasikilizaji milioni 1 ndani na nje ya Afrika Kusini.
Sasa basi, Radio ya Massiv Metro kwa kupitia +255 Global Radio ya Bongo, kwa mara ya kwanza siku hiyo ya Jumanne itazindua kipindi hicho kipya cha Afternoon Drive kikiongozwa na mtangazaji DJ Sbu na kitaruka kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku.
MJUE ZAIDI
DJ Sbu, mbali na ujasiriamali na utangazaji, pia amejikita kwenye elimu na ame kuwa akizu nguka katika shule mbali mbali nchini Afrika Kusini kutoa misaada ya kuwa some sha wana funzi mbali mbali na kuwasaidia wale wenye matatizo ya akili kupitia taasisi yake ya Sbusiso Leope Education Hadi sasa ameshatoa misaada ya kuwasomesha wanafunzi zaidi ya 500.
UHAMASISHAJI
Sbu pia ni mwandishi mzuri wa vitabu ambapo ana vitabu kadhaa kama Billionaires Under Construction ambacho hutumia katika majukwaa ya kuhamasisha watu kutafuta pesa. Amekuwa akipata mialiko mingi ya kuhamasisha katika shule na vyuo mbalimbali kama Harvard Business School, Massachusetts Institute of Technology (MIT) na University of Westminster vyote vya Uingereza.
Jarida la Forbes Afrika mwaka huu limemuweka kama kijana wa Kiafrika wa kuangaliwa zaidi huku Gazeti la Sunday Times, Mail na Guardian yakimtaja kuwa mmoja kati ya vijana 200 shupavu wajao. DJ Sbu amepata shavu pia katika kituo kikubwa cha TV Afrika cha CNBC ambapo ana kipindi kiitwacho Kicking Doors with Sbu Leope ambacho kinaelezea ujasiriamali na vipaji kwa vijana.
BURUDANI
Mkali huyu amejipatia umaarufu kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 2000 aliposhirikiana na mume wa memba wa Kundi la Mafikizolo, Nhlanhla, TK Nciza kufungua lebo kubwa ya muziki ya TS Records ikiwa ni muunganiko wa majina yao.
Lebo hiyo ambayo ipo Afrika Kusini imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwainua wasanii akiwemo mwanamuziki wa kike ambaye anaongoza kwa mauzo, Zahara. Yumo pia katika mafanikio ya muziki wa Kwaito kutokana na kuwakubali wasanii wa nyimbo hizo na kuwasaidia katika kuucheza muziki wao na kuutangaza ndani na nje ya Afrika Kusini.

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)