Ndege ya usaidizi ya mradi wa wanafunzi wa Afrika Kusini U-Dream yahusika katika ajali Tanzania

Admin
By -
0
Des Wernerkulia) na Werner Froneman (kushoto walikuwa katika ndege ya usaidizi ilioanguka Tanzania
Watu wawili walioanzisha mradi uliowafanya wanafunzi kupeleka ndege walioitengeneza katika mataifa mbalimbali barani Afrika wamefariki katika ajali ya ndege.
Raia wa Afrika Kusini Des Werner na Wener Froneman walikuwa wakiendesha ndege hiyo kutoka mji wa Cape Town kuelekea Cairo wakati ilipoanguka magharibi mwa Tanzania hapo jana tarehe 3 Agosti mwendo wa asubuhi.
Kulingana na vyombo vya habari nchini Tanzania ndege hiyo nyepesi ilianguka dakika moja baada ya kupaa angani kutoka katika uwanja wa ndege uliopo kijiji cha Igigwa Wilayani Sikonge Tabora magharibi mwa Tanzania.
Utawala wa eneo hilo unasema kuwa ndege hiyo iliharibika kabisa huku mabaki machache yakipatikana.
Ndege hiyo ilikuwa na abiria wawili pekee ambao wote walifariki.
Des Werrner na Werner Froneman walikuwa wakurugenzi wa U- Dream - mradi wa vijana wa Afrika Kusini kuendesha ndege iliotengenezwa nyumbani kutoka Capetown hadi Cairo.
Wanfunzi 20 walikamilisha kuunda ndege hiyo ndani ya wiki tatu
Walikamilisha safari yao mwezi uliopita - wakigonga vichwa vya habari ulimwenguni.
Ndege iliohusika katika ajali hiyo ni ya usaidizi wa mradi huo
Katika chapisho la mtandao wa facebook, U-Dream ilisema ilishangazwa na vifo vya wakurugenzi wake wawili.
Ndege hiyo iliotengenezwa mnamo mwezi Juni, ilisafiri katika mataifa tofauti ikiwemo, Misri, Namibia, Ethiopia na Zanzibar.
Wanafunzi hao walikuwa wakitoa mihadhara kwa wanafunzi wenzao kwenye kila nchi waliyosimama.
Ndege nyengine aina ya Sling 4, ilikuwa ikiandama nao na kuendeshwa na marubani wenye uzoefu ili kutoa msaada pale unapohitajika.
Baba wa Megan, Bwana Des Werner ambaye ni rubani mwandamizi alikuwa ni sehemu ya timu ya msaada.
Wanafunzi hao waliitengeneza ndege hiyo kwa wiki tatu kwa kuunganisha vifaa vilivyotengenezwa na kampuni moja nchini humo. Uundaji huo ulihusisha kuunganisha maelfu ya vifaa vidogo vidogo.

Changamoto walizokumbana nazo

Hata hivyo, mafanikio hayo hayakukosa changamoto, kulingana na Megan.
Huree!
Wanafunzi hao walikataliwa na mamlaka za Kenya kutua jijini Nairobi na ikabidi wabadili njia.
Katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, walichelewa kupata mafuta.
"Baada ya kuyapata, ndege ya pili ya msaada ikaanza kuvujisha mafuta na ikashindwa kuendelea na safari nasi na ikabaki marubani wawili tu mimi na Driaan van den Heever kuendelea na safari," ameeleza Megan.
"Tulikuwa na mashaka juu ya kupaa katika anga la Sudani kutokana machafuko ya kisiasa yanayoendelea."
Marubani hao sita wanafunzi walikuwa wakipokezana kurusha ndege hiyo.
Hata hivyo, aina ya leseni waliyopata ambayo ni daraja la kwanza pia ikawa kikwazo. Walitakiwa kutopaa juu sana na kufikia usawa wa mawingu.
Kipande cha mwisho cha safari kilikuwa ni mtihani mgumu kwa marubani hao.
"Tuliendesha ndege na Driaan van den Heever kwa saa 10 bila ya ndege ya usaidizi, ilikuwa ni wanafunzi wawili angai bila usaidzi wowote," ameeleza Megan.
Marubani wanafunzi (kutoka kkushoto) van den Heever, Werner na Hendrik Coetzer
Marubani hao wawili wanafunzi walipatwa na tatizo katika mifumo ya ndege hiyo muda mfupi baada ya kuingia kwenye anga ya Misri.
Hivyo wakafanya maamuzi ya kutua kwenye uwanja wa karibu zaidi badala ya ule wa Kimataifa wa Cairo kama ilivyokuwa imepangwa awali.
Nji iliotumiwa na ndege hiyo kutoka Capetown kuelekea Cairo
"Halai hiyo ilizua tafrani kidogo, lakini maamuzi yalifanyika kwa sababu za kiusalama," ameeleza Des Werner.
"Mwishowe tukagundua kuwa ilikuwa nyanya moja tu imecheza na wakairekebisha mara moja, lakini kukawa na urasimu mkubwa ambao ulichukua muda mrefu na kutakiwa na mamlaka waandike ripoti."
"Tulipotua Misri kwa dharura katika eneo la kwanza maafisa walitaka kutukamata, kutupokonya hati zetu za kusafiria na leseni lakini kwa bahati nzuri baada ya saa kama nne kila kitu kikawa sawa tukapata mafuta ya ziada ya kutufikisha Aswan, na kutoka hapo tukapaa mpaka hapa Cairo, lilikuwa ni jambo la furaha sana kutua Cairo," ameeleza Megan.



































































































































































































































































































































Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)