![]() |
| Damian Green, |
Naibu wa waziri mkuu wa Uingereza, Damian Green, ameachishwa kazi baada ya kubainika kuwa alikiuka kanuni za uwaziri.
Bwana Green ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Waziri mkuu Theresa May alibainika kuwa alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu picha za ngono zilizokutwa kwenye komputa yake ya ofisini
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amemlazimisha mmoja wa mawaziri wake wa ngazi za juu, Damien Green kujiuzulu hapo jana baada ya uchunguzi wa ndani kugundua kwamba alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu ngono ya mtandaoni katika ofisi yake bungeni.
Green alitiliwa mashaka pale gazeti la Sunday Times liliporipoti mwezi uliopita kwamba mnamo mwaka 2008 polisi waligundua ng'ono katika komputer yake ya ofisini ya Baraza la Wawakilishi la Uingereza.
Hata hivyo Waziri amekanusha kuhusika na mashitaka yote yanaomkabili.
Kujiuzulu kwa mmoja wa washirika wa kuaminika wa May, aliyemsaidia kukisogeza mbele chama chake kilichogawanyika, ni pigo kubwa akiwa yumo katika harakati za mwaka wa mwisho wa kujadili mchakato wa kujiondoa katika Umoja wa Ulaya unaojulikana kama Brexit na unaotarajiwa kumalizika mwaka 2019.
Tags
VITUKO
