KAMPUNI YA APPLE YAKIRI KUPUNGUZA UWEZO WA SIMU ZA IPHONE

Image result for picha za iphone 6
Kampuni ya Apple imekiri wasiwasi uliokuwa na wamiliki wengi wa simu ya iPhone kwa kufichua kwamba imekuwa ikizipunguza kasi baadhi ya simu za zamani za Iphone.
Wateja wengi kwa muda mrefu wamekuwa na wasiwasi kwamba kampuni hiyo inapunguza kasi ya kupakia na kupakua ya simu za zamani wakati zinapoendelea kuzeeka kwa sababu betri ya simu hizo zinapungua nguvu kila wakati simu hizo zinapoendelea kuzeeka.
Betri za lithium hupunguza nguvi zikiendelea kutumika
Betri za lithium hupunguza nguvi zikiendelea kutumika
Apple imesema kuwa lengo lake lilikuwa kuimarisha maisha ya simu hizo kwa wateja wao.
Kitendo hicho kilithibitishwa baada ya mteja mmoja kusambaza utendakazi wake katika programu ya Reddit, akisema kuwa iPhone 6S imepunguza kasi kubwa kutokana na kuzeeka lakini ikaongeza kasi hiyo muda mfupi baada ya kuwekwa betri mpya

Post a Comment

Previous Post Next Post