AMUUA MKE WAKE BAADA YA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI SIKU YA KRISMASI

POLISI Nchini Uganda wanamshikilia mwanaume mmoja aliyemuua Mke wake kwa kutumia panga akidai kachelewa kurudi nyumbani siku ya siku kuu ya Christmass.

Mwanaume huyo amesema Mkewe Betty Anyokoti ambaye aliondoka na kwenda kijijini kwao kusherehea sikukuu lakini alishangazwa alipoona mke wake anachelewa kurudi nyumbani ndipo akapatwa na hasira.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kinasema jirani yao ambaye amefahamika kwa jina la Okunyuku alisema majira ya saa nne usiku walimuona mwanaume huyo akizuunguka huku na kule kumtafuta mke wake .

Alieleza baada ya kumtafuta pale nyumbani na kutomuona alienda huko barabarani na kumpata ambapo walisikia makelele ya mabishanao ya wawili hao wakigombana na baadae walipotoka waliona mwanaume huyo kashika panga na keshamkata mke wake.

Polisi wanamshikilia mtu huyo kwa mahojiano na mwili wa mareehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Iganga ili uweze kufanyiwa uchunguzi zaidi.

TAZAMA HAPA KAULI YA MWAKA ALIYO ITOA JOTI KWA WANAWAKE

Post a Comment

Previous Post Next Post