SIMBA YAMKELA MGOSI AFANYA MAAMUZI YA AJABU


MUSSA Hassan ‘Mgosi’ amezua kali ya mwaka baada ya kustaafu soka na kurejea tena uwanjani. Inashangaza sana.

Mgosi alitundika daluga mwaka jana na kupewa umeneja wa klabu ya Simba lakini kitendo cha mabosi wa timu hiyo kumhamishia kwenye timu ya vijana ni kama kilimkera na kumfanya arejee uwanjani.

Nahodha huyo wa zamani wa Simba amejiunga na Dodoma FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na ataanza kuonekana uwanjani mara tu mzunguko wa pili wa ligi hiyo utakapoanza.

Unafikiri Mgosi ni mchezaji wa kwanza kutangaza kustaafu soka na kisha kurejea uwanjani? Hapana, wapo wachezaji wengi tu wa Bongo waliobatilisha uamuzi wao wa kustaafu na kurejea uwanjani.

Emmanuel Gabriel

Straika mtata aliyefahamika kama Batigol alipata mafanikio makubwa akiwa na Simba, naye alitundika daluga na kisha kurejea uwanjani.

Gabriel aliyekuwa akisifika kwa kuwatesa mabeki na kufumania nyavu, alitamba na Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000 kabla ya baadaye kutimka klabuni hapo na kuamua kujiweka pembeni na mchezo huo pendwa nchini.

Wakati mashabiki wa soka wakiamini staa huyo atakuwa tayari amejikita kwenye shughuli nyingine, Gabriel alibuka mwaka jana na kujiunga na Friends Rangers inayoshiriki FDL. Bahati mbaya staa huyo alishindwa kuitumikia vilivyo timu hiyo kutokana na majeraha.

Fred Mbuna

Nyota wa zamani wa Yanga, Fred Mbuna naye aliamua kubatilisha maamuzi yake ya kustaafu soka na kurejea tena uwanjani.

Mbuna aliyeichezea Yanga kwa miaka 11 alitundika daluga mwaka 2012 na kufanyiwa sherehe ya kuagwa Jangwani wakiamini muda wake kwenye soka umekwisha, lakini aliamua kurejea tena uwanjani.

Nahodha huyo wa zamani wa Yanga alipumzika kwa mwaka mmoja tu na kisha kujiunga na Majimaji ya Songea aliyoipambania tangu ikiwa FDL mpaka ikapanda Ligi Kuu.

Mbuna aliteuliwa tena kuwa nahodha wa Majimaji akicheza kwa mafanikio msimu wa 2015/16 na kuisaidia isishuke daraja. Mpaka sasa haifahamiki kama Mbuna amestaafu ama atarejea uwanjani tena.

Ulimboka Mwakingwe

Mchezaji mwingine wa maana aliyestaafu soka na kisha kurejea uwanjani ni Ulimboka Mwakingwe. Winga huyo wa zamani wa Simba aliamua kujiweka pembeni na soka lakini ilipotokea fursa alirejea tena uwanjani.

Ulimboka alicheza Simba kwa miaka zaidi ya tisa kisha kuamua kustaafu mwaka 2011 lakini miaka minne baadaye alirejea tena uwanjani na kuamua kukinukisha tena.

Awamu hii staa huyo wa zamani wa Taifa Stars alijiunga na Burkina Faso ya kwao Morogoro iliyokuwa ikishiriki FDL. Bahati mbaya kwa Ulimboka ni kwamba hakuweza kuitumikia vilivyo timu hiyo kutokana na majeraha. Burkina Faso ilishuka daraja msimu huo wa 2015/16 na sasa inashiriki Ligi daraja la pili.

Abuu Mtiro

Beki bora zaidi wa kushoto kuwahi kutokea kwenye kikosi cha Yanga kwa miaka ya karibuni, Abubakar Mtiro naye alistaafu soka na kurejea tena uwanjani.

Mtiro aliyejiunga na Yanga mwanzoni mwa miaka ya 2000 na kuichezea kwa mafanikio makubwa ikiwemo kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu Bara, alitundika daluga na kurejea tena uwanjani.

Baada ya kuondoka Yanga mwaka 2009, Mtiro alikwenda kucheza soka la kulipwa huko Msumbiji ambako alidumu kwa miaka mitatu kabla ya kurejea nchini na kuendelea na shughuli zake.

Mwaka 2013, Mtiro alihamasika tena kurejea uwanjani na kujiunga na Ashanti United ambayo aliitumikia kwa nusu msimu tena akiwa mchezaji wa kudumu katika kikosi cha kwanza.

Kutokana na kiwango chake imara alisajiliwa na Kagera Sugar mwaka 2014 na alikwenda kupandisha makali yake na kufanikiwa kuitwa tena kikosi cha Taifa Stars.

Shadrack Nsajigwa

Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa naye kabla ya kutuliza akili, alistaafu na kurejea tena uwanjani.

Nsajigwa alistaafu soka mwaka 2012 katika klabu yake ya Yanga na Taifa Stars. Nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Stars aliamua kujiweka pembeni baada ya kuitumikia Yanga kwa mafanikio na kushinda mataji zaidi ya sita tofauti.

Mara tu baada ya kustaafu soka, Nsajigwa alipata kazi ya kuinoa Lipuli ya Iringa iliyokuwa ikishiriki Ligi daraja la Kwanza, lakini aliikacha timu

TAZAMA HAPA MUIMBA KWAYA WA AJABU KUTOKA KENYA

Post a Comment

Previous Post Next Post