WATU 41 WAMEUAWA KWA SAMBULIO LA KIGAIDI NCHINI AFGHANSTAN, IS YAKIRI KUHUSIKA

media


Watu 41 wameuawa leo katika shambulizi lililiofanywa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS katika kituo kimoja cha utamaduni wa Washia mjini Kabul.
 Wizara ya Afya ya Afghanistan imesema wanaume 35, wanawake wanne na watoto wawili ni miongoni mwa waliokufa.
 Msemaji wa wizara hiyo amesema watu wengine 84 pia wamejeruhiwa katika shambulizi hilo. 
Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema mlipuaji wa kujitoa muhanga alijilipua nje ya kituo hicho kabla ya milipuko mingine miwili midogo kutokea wakati watu walipokusanyika kuwasaidia waathiriwa. 
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na Kiongozi Mtendaji Abdullah Abdullah, pamoja na Kikosi cha NATO nchini humo, wamelaani shambulizi hilo. 
Wanamgambo hao wa Kisuni wameimarisha mashambulizi yao dhidi ya Washia hasa mjini Kabul.
 Katika mwezi wa Oktoba, watu 71 waliuawa na wengine 90 wakajeruhiwa katika shambulizi la IS kwenye msikiti mmoja wa Kishia.

Post a Comment

Previous Post Next Post