Kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis |
Kabla ya kupanda ndege kuelekea nchini humo hapo jana, Papa Francis aliwaomba waumini wa Kikatoliki kumuweka katika maombi ili kuwepo kwake Myanmar kuwe ishara ya matumaini na kuimarisha udugu.
Wananchi wengi wanaham ya kusikia kama kiongozi huyo wa kidini atatumia neno "Rohingya" kuwaita kundi la watu wanaosema wamenyanyaswa.
Maafisa nchini Myanmar wanakataa kulitumia jina hilo, jambo ambalo linaongeza wasiwasi kwamba huenda kukazuka ghasia za Mabudda walio wengi nchini humo iwapo Papa atalitumia jina hilo.
Hata kabla ya kuondoka Roma, Papa Francis alikuwa anakabailiwana kitendawili cha kidiplomasia: iwapo kuliita kundi dogo la waislamu Myanmar - Rohingya.
Zaidi ya Warohingya laki sita wamelazimika kukimbia kutoka jimbo la Rakhine nchini Myanmar tangu mwezi Agosti kutokana na ghasia ambazo Umoja wa Mataifa na Marekani zimezitaja kuwa zinazolenga kuwaangamiza watu wa jamii fulani.
Papa ambaye atafanya ziara ya siku sita nchini Myanmar na Bangladesh anatafuta kuhimiza maridhiano na majadiliano ili kuutatua mzozo huo.
Atakutana na Kiongozi wa Myanmar, Aung Suu Kyi na mkuu wa majeshi Min Aung Hlaing.