MENEJA KAMPENI WA CHADEMA APANDISHWA KIZIMBANI


Mwanza. Viongozi na wanachama 17 wa Chadema wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza, wakikabiliwa na makosa ya kufanya vurugu na kujeruhi wakati wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Mhandu jijini Mwanza.

Uchaguzi mdogo wa udiwani ulifanyika Jumapili Novemba 26,2017 katika kata hiyo, ikiwa miongoni mwa 43 nchini zilizofanya uchaguzi.

Miongoni mwao wamo aliyekuwa meneja kampeni wa Chadema wa kata hiyo, Charles Chinchebela na mjumbe wa kamati tendaji ya chama hicho Ilemela, Emmanuel Tumbo.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani leo Jumatano Novemba 29,2017 na wanasubiri kusomewa mashtaka.

Ingawa hajapatikana leo kuzungumzia suala hilo baada ya aliyepokea simu kueleza yuko kwenye kikao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi Jumatatu Novemba 27,2017 alisema wanawashikilia watu 17 kwa makosa mbalimbali kuhusu uchaguzi huo mdogo wa udiwani ulioisha kwa mgombea wa CCM kuibuka mshindi.

Post a Comment

Previous Post Next Post