Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mkoani morogoro
tukio hilo limetokea kwenye kijiji cha nyalutanga mkoani morogoro baada ya askari polisi kuwafyatulia lisasi wananchi
katika tukio hilo watu wawili wamefariki dunia ambao wametambuliwa kwa majina ya ramadhan kimege na kibwana msipwile huku raia mmoja akijeruhiwa kwenye makalio ambae amefahamika kwa jina la ismahil msagare
mkuu wa wilaya amesema chanzo cha tukio hilo ni mala baada ya mifugo kuingia sehemu isiyo takiwa ndipo askari mgambo wakaenda kuikamata hatua iyo zusha mvutano
miongoni mwa askari mgambo alisema baada ya kwenda kuikamata mifugo hiyo ndipo wananchi wakaanza kuwazonga huku wakijaribu kuipola bunduki ambayo alikuwa nayo askari polisi
baada ya wananchi kumzidi nguvu askari aliamua kufyatua risasi kujinusuru ambapo kwa bahati mbaya zikawakuta wananchi wawili na kumjeruhi mtu mkoja kwenye makalio
mkuu wa wilaya amesema ameunda kamati maalumu kuchunguza undani wa tukio hilo la watu kupoteza maisha