WATU 6 FAMILIA MOJA WAHUKUMIWA KUNYONGWA SUMBAWANGA

Watu sita wa familia moja wahukumiwa adhabu ya kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kumuua ndugu yao wakimtuhumu mchawi

ukumu hiyo imetolewa katika mahakama wilayani sumbawanga chini ya hakimu Adam mambi baada ya kujilizisha na ushahidi ilio letwa na upande wa mashitaka

watu walio hukumiwa ni
Ferdnand kamande
Peter mpandisharo
Edes kamande
Stephen sikanda
Henrick guvumali
Antory kamande
pia katika kesi hiyo ndugu wawili waliachiwa baada ya kukutikana hawana hatia ambao ni
Elistid kamande na Wilbord kamande

watu hao walitenda kosa hilo september 27 mwaka 2014 ambapo walienda nyumbani kwa marehemu kisha wakachoma moto nyumba ya marehemu huku marehemu akikimbia nyumba yake

baada ya kuchoma nyumba walimtafuta kisha wakamkamata na wakampiga na hatimae wakamchoma moto wakimtuhumu kuwa ni mchawi

mahakama baada ya kusikiliza pande zote mbili ikaamua kutoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine wenye imani potofu kama hizi

Post a Comment

Previous Post Next Post