IDADI YAWATANZANIA WANAO NGOJA KUNYONGWA WAFIKIA 447

Kwa mujibu wa takwimu ya haki za binadamu imesema idadi ya watanzania wanao ngojea kunyongwa wafikia 447 huku kati yao wanawake ni 20

idadi hii imekuwa kubwa baada ya adhabu ya kifo kuto fanyika tangu mwaka 1994

idadi hii imekuja baada ya mahakama mkoani Rukwa kuwahukumu adhabu ya kifo watu wawili hapo jana

katika kesi hiyo mahakama mkoani rukwa imewahukumu kunyongwa watu wawili wakazi wa kijiji cha kaengesa mkoani rukwa Maurus semwanza na Edwars chekwama baada ya kumbaka na kisha kumuua Magreth razaro

tukio hilo lilifanyika majira ya saa 4:00 usiku baada ya marehemu ambae alikuwa akinywa pombe ya kienyeji kwenda kichakani kujisaidia ndipo watu hao wakambaka na kisha kumweka kitu chenye ncha kari sehemu za siri hatua iliyopelekea kutoka utumbo nje

baada yatukio hilo marwhemu akiwa hari mbaya aliomba msaada na wasamalia wakaja kumsaidia huku akiwa anawakumbuka watuhumiwa lakini baadae alifariki

Post a Comment

Previous Post Next Post