LORI LA DANGOTE LAKAMATWA LIKIWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU

Idara ya uhamiaji mjini dar es salaam imelikamata lori la kampuni ya dangote likiwa limebeba wahamiaji haramu

wahamiaji haramu hao wanne raia wa Ethiopia walikamatwa maeneo ya kongowe mjini dar es salaam wakielekea mkoani mtwara

pia uhamiaji.imewashika watu waliokuwa wakilisindikiza gari hilo huku wakiwa kwenye gari aina ya toyota passo

mkuu wa uhamiaji amesema wahamiaji hao haramu walikamatwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamalia wema na kuwakuta wakiwa na tiketi zikionesha wanatoka msata wanaelekea dar es salaam

pia uhamiaji umetoa onyo kwa wenye nyumba za wageni kwakuwa zimekuwa zikitumika kuwaficha wahamiaji haramu

Post a Comment

Previous Post Next Post