Mwanamke aliye fahamika kwa jina la zena mohamed (29) anashikiliwa.na polisi baada ya kumuuwa kwa kisu.mume wake aliye tambulika kwa jina la bakar salehe(35)
tukio hili limetokea kwenye mtaa wa malange mkoani shinyanga siku ya jana tarehe 20.septemba 2017 majira ya saa mbili usiku
akiongea na wana habari mkuu wa polisi amesibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akisema ugomvi huo ulikuwa ni wa wivu wa mapenzi
kwa mujibu wa maelezo mwanamke huyo alipokea simu ya mume wake na kusikia sauti ya mwanamke hatua iliyo mfanya kuhisi kuwa ni hawala wa mume wake
kufuatia hatua hii ulizuka ugomvi na hatimae jioni mwanamke huyo alimvizia mume wake akiwa amelala ndipo akamjerui na kisu mpaka kufa
baada ya kufanya tukio hilo mwanamke huyo alifungua sauti kubwa ya redio kisha kufunga mlango na kukimbilia shinyanga mjini kwa mama yake
baada ya kufika huku akiwa amechanganyikiwa akamwambia mama yake kuwa amesababisha mauaji ndipo mama yake akapiga simu polisi na kutoa taarifa na hatimae mwanamke huyo kukamatwa.