DENI LA TAIFA KWENYE MATIBABU NJE YA NCHI LAFIKIA BILIONI 34

waziri wa afya Ummy mwalimu asema deni la taifa nje ya nchi lililotokana na matibabu lafikia bilioni 34

akiongea na wana habari amesema serikali imekuwa ikitoa garama nyingi kugharamia watu kwenda kutibiwa nje wakati matatizo hayo nchini yanatibika

amesema pia ni marufuku kwa hospitali ya muhimbili kuruhusu mtu akatibiwe nje kama ugonjwa alionao waweza kutibika nchini

pia kasema kwa wale wenye pesa zao wapo ruksa kwenda ila hii ni kwa wanao tibiwa kwa pesa za serikali

amesema Tanzania imesomesha madaktari wengi sasa ni muda muhafaka kuwatumia katika kupunguza gharama zisizo za lazima

deni hilo ni la miaka minne iliyopita na kwasasa hawaitaji kulikuza tena deni hilo bila ya sababu

Post a Comment

Previous Post Next Post