Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya watu kushambulia kwa bunduki waumini waliokuwa wakitoka msikitini
tukio hilo limetokea kusini mwa ufaransa katika msikiti wa Arrahma ambapo watu wawili wakiwa na bunduki mkononi walivamia watu waliokuwa wakitoka katika ibada ya jioni
watu wanne wa familia moja walishambuliwa kwa risasi akiwemo mtoto mdogo wa kike wa umri wa miaka saba alijeruhiwa
mpaka sasa majeruhi nane wapo hospitali wakipatiwa matibabu huku walio sababisha tukio hilo wakiwa hawajakamatwa mpaka sasa
polisi imesema tukio hilo si la kigaidi ni tukio tu lenye kuonesha chuki za kidini na polisi wanaendelea na uchunguzi ili wawakamate waliofanya tukio hilo
kwa mujibu wa mashuhuda walisema watu walianza kukimbia baada ya kuwaona watu wawili wakishuka kutoka kwenye gari wakiwa na bunduki mkononi ambapo mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu vifo vyovyote
Tags
Kimataifa