Hivi karibuni kumekuwa na wimbi la wanachama na madiwani mkoani arusha ambao wanatangaza kuhama chama cha demokrasia na maendeleo chadema na kuhamia cccm
mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Aman golugwe amesema wanao tamani kuhama wahame mapema wasichelewe kwa kuwa wanafaham kuna wengine wapo wanampango wa kuhama kutoka katika chama hicho
miongoni mwa madiwani walio hama kutoka chadema mkoani arusha ni pamoja na Credo kifukwe kata ya mutiet,Anderson sikawe kata ya legaluki, Emanuel.moleli kata ya makiba , Greyson isagya kata ya maroron na Josephine mshiu wa viti maalum
mwenyekiti amesema wengi wanahama na hawaathiri chochote katika chama na wenye mpango wa kuhama wahame
pia mbunge wa Arusha mjinj Godbless lema alisema wengi wanao hama wanahama kwa uroho wa madaraka na ushawishi wa fedha kauli iliyo kanushwa na madiwani hao
katika mwaka wa uchaguzi mkoani arusha mwaka wa 2015 ulikuwa mzuri kwao kwakuwa waliweza kushinda majimbo sita kati ya saba na kuchukuwa kata tano kati ya saba na kuunda halmashauri.
Tags
Kitaifa