
Mahakama ya hakimu mfawizi wilaya ya sengerema imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la ujangili
katika kesi ya kwanza Antoni sahana amehukumiwa kwemda jela miaka 20 baada ya kukutwa na mzoga wa pundamilia wenye thamani ya shilingi 2616000 ambao alitoka nao katika mbuga ya wanyama ya serengeti
katika kesi nyingine mtuhumiwa chacha kirarya miaka 56 na Samuel kisume wamehukumiwa miaka 20 kila mmoja baada ya kukutwa na miguu mitatu ya nyumbu wenye thamani ya shilingi 1430000 ambao waliuawa katika mbuga ya wanyama ya serengeti
hakimu alisema alitoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa wengine wanao penda kuuwa wa nyama mbugani maana ni kosa kisheria kukutwa na nyara za serikali
lakini watuhumiwa Samueli na Chacha waliomba kupunguziwa adhabu kwakuwa walifanya hivyo kwaajili ya ugumu wa maisha lakini mahakama haikuwasikiliza hivyo wata tumikia kifungo chao
Tags
Kitaifa