Watanzania zaidi ya elfumoja wapo magerezani nchi tofauti duniani baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya
wengi wao wamekamatwa nchi za china na afrika ya kisini ambapo baadhi ya waliokamatwa wanasubilia adhabu ya kifo kutokana na kukutwa na madawa ya kulevya
mfano nchi kama ya china wao huwa na sheria kali kupambana na madawa ya kulevya ambapo ukikamatwa adhabu huwa miaka kumi au kunyongwa ambapo muda mwingine huweza kukupa adhabu ya kupigwa risasi mbale za watu ili iwe fundisho kwa wengine
lakini ingawa na haya yoote vijana bado wana rubunika na kusafilisha madawa haya haramu ambayo ukikamatwa adhabu yake huwa ni kubwa saana
pia katika njia za kusafilisha walio wengi hutumia njia ya kumeza ambayo muda mwingine huwa sababishia matatizo hasa pale yanapo pasuka yakiwa tumboni mbebaji hupoteza maisha
hivyo ni vizuri serikali ikajitahidi kutoa elimu kwa vijana kwa kuwa wao ndiyo wahanga wakubwa wa biashara hii ambayo hupoteza nguvu kazi ya taifa kila siku
Tags
Kitaifa