MWIJAGE ASEMA WANAO ULIZIA SERIKALI KUKATAZA KUUZA MAHINDI NJE NI WASHAMBA



Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji mh Charles mwijage asema wanao shangaa serikali kukataza kuuza mahindi nje ni washamba

akiongea na wanahabari waziri mwijage alisema wanao shangaa kukatazwa kwa kuuzwa mahindi nje ya nchi ni washamba kwakuwa hawajui dhima ya viwanda

alisema haiwezekani tunauza mahindi alafu wana tuuzia pumba wakati mahindi tulilima wenyewe

alisema ni haeli tukauza unga na siyo mahindi kwakuwa viwanda vyetu vitakosa malighafi na hatimae kufungwa kitu ambacho serikali haitaki kitokee

pia mwijage amesema wapo mbioni kujenga kiwanda cha matunda mjini tanga kwakuwa matunda mengi kutoka tanga yanasafilishwa kwenda nje alafu baadae wana tuuzia sharubati ya matunda yetu wenyewe

hatua hii imekuja baada ya taarifa kupitia waziri mkuu ya kuto ruhusu uuzwaji na usafilishwaji wa mahindi kwenda nje ya nchi wakati taifa bado lina uhitaji wa chakula

serikali imeamua kupiga marufuku kwakuwa kipindi cha masika baadhi ya maeneo nchini yalikosa mvua hatua ambayo inaweza kupelekea kutokea kwa upungufu wa chakula


Post a Comment

Previous Post Next Post