
Jeshi la polisi mkoani rukwa ina mshikilia mwalimu wa shule ya sekondari ya Miangala baada ya kumpa ujauzito mwanafunzi
mwanafunzi huyo wa miaka 16 ambae anasoma kidato cha tatu katika shule hiyo alianza kuhisiwa kuwa ni mjamzito na alipo fanyiwa vipimo na akakutwa na ujauzito wa miezi mitatu
mkuu wa shule hiyo amesibitisha mwalimu wake kufanya kitendo hicho na alisema alimuonya lakini mwalimu huyo hakusikia ushauri
mzazi wa binti huyo anasema ameumia kupata taarifa hizo na kibaya yeye hana uwezo wa kumpeleka mwanae shule binafsi na hajui kama mwanae atasoma tena
polisi imesibitisha kumshikilia mwalimu huyo baada ya kumpatia ujauzito mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu
Tags
Kitaifa