MTOTO ALIWA NA FISI WAKATI AKINGOJA CHAKURA MWANZA



Siku ya tarehe 23 mwezi july mtoto mdogo aliwa na fisi wakati akisubiri chakula cha jioni nyumbani kwao

Tukio hili limetokea katika kijiji cha Izizimba mkoani mwanza ambapo mtoto wa miaka minne aliye fahamika kwa jina la Limi Bunzama ameliwa na fisi karibu na nyumbani kwao

mtoto huyo alikuwa akicheza nje ya nyumba yao akisubiri chakula ghafla akaja fisi huyo na kumbeba kisha kwenda nae polini

baada ya muda mama wa mtoto akashtuka ndipo akaanza kumsaka akisaidiana na wanakijiji ndipo wakamkuta akiwa ameliwa sehemu kubwa ya mwili wake huku fisi akiwa ametoweka

baada ya tukio hilo wanakijiji waliamua kuanza kumtafuta fisi huyo lakini mpaka sasa hawajafanikiwa kumpata huku mtoto akiwa amesha fariki


Post a Comment

Previous Post Next Post