MDEE ATAKA CHADEMA KUWARUDISHA SHULE WALIOPATA MIMBA KATIKA HALMASHAULI WANAZO ZISHIKILIA

Mbunge wa kawe kupitia chadema Halima mdee awataka chadema kuwasaidia kuludi shule wasichana waliopata ujauzito waishio kwenye halmashauri wanazo ziongoza

Mdee akiongea kwenye mkutano na wana habari alisema niwajibu wa mtoto kupata elimu hivyo basi chadema waoneshe mfano wa kuwasaidia waishio kwenye halmashauri zilizo chini yao

alisema wanatakiwa kuwahimiza kuludi shule bila kujari maneno ya mh raisi kwa  kuwa ni haki ya mtoto yoyote kupata elimu ili imsaidia kujikomboa katika maisha yake ya kikasiku

kauli hii ya mdee imekuja baada ya raisi kusisitiza kuwa binti atakae pata ujauzito shuleni afukuzwe na asiruhusiwe kurudi shuleni kwa kuwa serikali haijajipanga kuwasomesha wazazi

kauli hii ya raisi imeleta mjadara mkubwa huku baadhi ya watanzania wa jinsia zote wakiipinga kwakuwa inamyima haki mtoto wa kike ya kupata elimu kwakuwa kuna baadhi ya wanafunzi hupata mimba baada ya kubakwa na siyo kwa makusudi


Post a Comment

Previous Post Next Post