AKAMATWA NA PEMBE ZA NDOVU MJINI MOROGORO

Polisi mkoani Morogoro inamshikilia bwana kimaso kibena miaka43 mkazi wa mlali baada ya kukutwa na pembe za ndovu za thamani ya shilingi milioni 33

kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa polisi alipoongea na wana habari alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa doria

baada ya polisi kupata taarifa za kiinterejensia waliamua kufanya upalelezi na baadae kwenda kupekua kwenye nyumba ya mtuhumiwa maeneo ya mlali ndipo wakafanikiwa kukamata pembe hizo zikiwa katika mfuko wa salfeti

pia baada ya uchunguzi ndani ya nyumba hiyo wamefanikiwa kupata pikipiki mbili aina ya SUNLG ambazo bado zinachunguzwa


Post a Comment

Previous Post Next Post