MADEREVA 18 WA TANZANIA WATEKWA DRC

Madereva 21 wakiwemo watanzania 18 wametekwa nchini DRC juni 29

madereva hao wa kampuni ya ALISTAIR walitekwa juni ya 29 nchini kongo ambako walikuwa wakisindikizwa na wanajeshi wa DRC lakini baada ya kuvamiwa na waasi wanajeshi wa serikali walizidiwa nguvu ndipo wakatekwa

kwa mujibu wa meneja wa kampuni Joyce mbise alisema miongoni mwa madereva hao watatu ni waganda na waliobaki ni watanzania

madereva hao walitekwa katika kijiji cha lulimba kati ya ziwa tanganyika na kindu

pia amesema wameongea na waasi hao na wameambiwa afya za madereva hao ziko sawa na hawana tatizo lolote lilie na wamesema hawata wadhuru kwakuwa wao hawana ugomvi na hawa madereva ugomvi walionao ni dhidi ya serikali ya DRC

pia wamewaambia kuwa miongoni mwa gari zao tatu zimeharibika vibaya kufuatia kurushiana kwa risasi baina ya waasi hao na jeshi la serikali

pia meneja amesema wamesha toa taarifa kwa vyombo husika ili taratibu za kuwapata madereva hao zifanyike

habari ya kutekwa kwa madereva nchini kongo hii si mala ya kwanza miezi kadhaa iliyopita madereva wengine kutoka tanzania nao walitekwa nchini kongo na baadhi ya magari yalichomwa moto katika tukio hilo


Post a Comment

Previous Post Next Post