Kijana aliye fahamika kwa jina la Benjamin zakalia miaka 22 amemuua mjomba wake Adam joseph miaka 30 akimdai gunia moja la alizeti
kwa mujibu wa taarifa ni kwamba siku ya tukio yaani jana usiku wa kuamkia leo kijana benjamini alfuata mjomba wake kwenye baa ya pombe baada ya kubishana kwa muda mrefu ndipo Benjamini akachomoa kisu na kumchoma Adam joseph na kutokana na majeraha makubwa Adam alifarika palepale
baada ya kusababisha tukio hili mtuhumiwa akaamua kutoroka na kutokomea kusiko julikana ambapo baada ya kutokea kwa tukio hilo wanakijiji wa ninga wilayani kalambe ambako tukio lilitokea walitoa taarifa polisi na polisi wanaendelea na uchunguzi ili wamkamate mtuhumiwa huyo
Tags
Kitaifa