DIWANI WA CHADEMA AJIUZURU NA KUHAMA CHAMA KWENDA CCM



Kumekuwa na mwendelezo wa madiwani na wanachama wa chadema kuhama chama na kuhamia ccm hasa mkoani arusha hatimae diwani mwingine atangaza kuhamia ccm

ni diwani wa kata ya ngabobo mkoani Arusha bwana Solomon laizer ametangaza kuhama chama na kuhamia ccm

diwani huyo amesema ameamua kuhama chama na kuhamia ccm kwakuwa amelizishwa na utendaji kazi wa rais magufuri tangu ashike madaraka

baada ya madiwani sita mkoani arusha kutangaza kuhama mbunge wa arusha mjini Godbless lema amesema kumekuwa na ushawishi unao fanyawa na ccm ili kuiua chadema arusha wakitumia pesa kuwalubuni baadhi ya madiwani kuhama chama hicho

pia chadema wamesema kuna kampeni ya kuiua chadema kwenye mikoa na majimbo wanayo yashikilia ambako pia katika jimbo la arumeru mkoani kikimanjaro madiwani watano wametangaza kuhama chama


Post a Comment

Previous Post Next Post