SERIKALI YAKILI UWEPO WA BANDARI BUBU NCHINI

Akijibu swali bungeni naibu waziri wa ujenzi na mawasiliano Edwin ngonyani amekili uwepo wa bandari bubu nyingi nchini

amesema bandari bubu nchini ni nyingi na zinasababisha upotevu mkubwa wa mapato pia ni vichochoro vya kupitishia biashara za magendo

pia amesema katika harakati za kuzitokomeza bandari hizi bubu si sirikali pekeyake hata wananchi wanatakiwa kuisaidia serikali katika jitihada hizi za kuzuia bandari bubu na bishara haramu zinazo fanyika humo

bandari bubu kwa miaka mingi zimekuwa njia pia za wahamiaji haramu kuingia na hata kutoka nchini hutumia bandari hizi kukwepa askari hivyo zinabidi kutokomezwa vinginevyo zitaendelea kuleta matatizo mengi


Post a Comment

Previous Post Next Post