Muvi ya Irene Uwoya na Msami imeshindikana kutoka,Kisa hiki hapa..

Msanii wa bongo Fleva ambaye pia ni dancer maarufu ,Msami amesema amesikitishwa na kitendo cha muvi yake aliyofanya na Irene Uwoya kutotoka mpaka leo kwani anahisi kama amepoteza muda wake wa bure kwenye mradi huo.
Msami amefunguka kuwa muvi hiyo iliyofanyika Afrika kusini inashindikana kutoka kwa sababu ya kutokuwepo na maelewano mazuri kati ya Irene Uwoya na John Kalage ambaye ndiye director wa muvi hiyo.
Kuna matatizo katikati hapa kati ya director na Uwoya,director ndiye anasabisha muvi isitoke .Kiukweli mimi mwenyewe nimekuwa disappointed kwa kuwa nahisi nimepoteza muda wangu bure“alifunguka Msami na kusema kuwa imekuwa kawaida watu kugombana na Kalage na hajui tatizo ni nini?
Source:clouds

Post a Comment

Previous Post Next Post