MTOTO WA MIAKA MITANO ABAKWA MWANZA

Mtoto mmoja wa umri wa miaka mitano amebakwa na kijana ambae jina lake limeifadhiwa kisha kijana huyo kutoroka

mkuu wa polisi mkoa wa mwanza Ahmed msangi amesibitisha kutokea tukio hilo lililotokea maeneo ya kilumba ilemela mkoani mwanza

kwa mujibu wa mashuhuda mtoto huyo alibakwa na huyo kijana hatua iliyo mpelekea kupata maumivu makubwa kutokana na kitendo hicho

polisi bado inaendelea na uchunguzi kumtia nguvuni kijana huyo ambae baada ya kufanya tukio hilo alifanikiwa kutoweka na hakulikani alipo mpaka muda huu

matukio ya ubakaji watoto ni mengi nchini huku baadhi ya watu wakiyausisha na imani za kishilikina


Post a Comment

Previous Post Next Post